Monday, November 25, 2013

STORIA FUPI KUHUSU BLANDINA CHANGULA (JOHARI)

BLANDINA CHANGULA (JOHARI)


       Jina la Kiraia    Blandina Changula
      Jina la Kisanii   Johari
      Nchi                   Tanzania
      Alizaliwa            27 Julai 1983
      Kazi yake          Muigizaji       
Blandina alipata elimu ya msingi katika shule ya Bugoyi mwaka 1990 hadi 1997 na kujiunga katika shule ya sekondari ya kutwa ya Buluba iliyopo Shinyanga mwaka 1998 hadi 1999.
Akiwa kidato cha pili alihamishiwa katika shule ya bweni ya Kanawa hukohuko mkoani Shinyanga mwaka 1999 hadi 2000 na mwaka huo huo baada ya kuingia kidato cha tatu akahamishiwa tena jijini Dar es Salaam katika shule ya Greens iliyokuwa maeneo ya Temeke kabla ya kuhamishiwa Ubungo shule ambayo alimalizia kidato cha nne hiyo ilikuwa mnamo mwaka 2001.

No comments:

Post a Comment